Miss Ilala 2013 Doris Mollel akitia
saini kitabu cha wageni katika shule ya msingi Tabata Jika wakati
alipotembelea shuleni hapo na kukabidhi vitabu vya maandalizi ya mtihani
wa Darasa la 7.
Doris Mollel, Miss Ilala 2013
akimkabidhi baadhi ya Vitabu mkuu wa shule ya msingi Tabata Jika Bwana
Kiwia. Kushoto ni katibu wa kamati ya Miss Tabata 2013 Bw. Adili.
Miss Ilala 2013 Doris Mollel akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na walimu wa shule ya
msingi Tabata Jika baada ya kukabidhi Vitabu shule hapo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi
Tabata Jika wakiwa katika picha ya pamoja na Miss Ilala 2013 Doris
Mollel, huku wakiwa na baadhi ya vitabu vilivyokabidhiwa shuleni hapo na
mrembo huyo.
No comments:
Post a Comment